.Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limeungana na United Nations Children’s Fund (UNICEF) pamoja na vikundi mbalimbali vya hamasa ikiwa ni pamoja na jamii kuadhimisha siku ya mtoto wa kike Duniani.
Maadhimisho hayo yalifanyika Oktoba 11, 2024 Stendi ya mabasi ya Mlowo ambapo Koplo wa Polisi Gladness kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Wilayani Mbozi alitoa elimu ya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto, Pia aliwaelekeza watoto wa kike walioudhuria hafla hiyo kuwa siku hii ni siku muhimu kwao ambayo huwakumbusha Watoto wa kike juu ya haki zao za Msingi ikiwemo haki ya kupata Elimu, pia kama Watoto wakike wanao wajibu wa kufahamu haki zao ambazo kimsingi ni hatma ya maisha yao.
Naye, Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Songwe Bi. Tumaini Kibona amesema siku hii itumike kama chachu ya kuendelea kupata haki za Msingi za Watoto wa kike na kutambua changamoto ili kuweza kuzitatua kwa kutoa taarifa kwenye taasisi husika na vingozi katika maeneo wanayoishi ili ziweze kushughulikiwa kwa haraka.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Songwe Bw. Martin Shigela aliwasisitiza kuwa usalama wao ni muhimu kwa maendeleo ya maisha yao na taifa kiujumla kwahiyo aliwataka wasisitishe ndoto zao kwa kutokutoa taarifa za ukatili wanazokumbana nazo katika maeneo yao hivyo mnatakiwa kutoa taarifa kwa Taasisi na mamlaka husika katika kulinda haki na ustawi wa maendeleo ya mtoto wa kike ili waweze kutimiza malengo ya masomo na maisha yao ya baadae.
This post was created with our nice and easy submission form. Create your post!
GIPHY App Key not set. Please check settings