in

KAMPENI YA”TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA” YAZINDULIWA SHINYANGA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Oktoba 18, 2024 limezindua kampeni ya “Tuwaambie kabla hawajaharibiwa” yenye lengo la kufikisha ujumbe kwa wanafunzi wote wa Shule za msingi, Sekondari na vyuo vya kati mkoani humo.

Kampeni hiyo imezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude ambapo amelipongeza Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha dawati la Jinsia na watoto kwa kubuni na kuzindua kampeni hiyo yenye lengo la kuwajengea uwezo watoto na vijana kuweza kutambua hatari na kuchukua tahadhari ili wasijiunge katika makundi ambayo yanaweza kupelekea kutofikia ndoto zao.

Aidha Mhe. Mkude aliwakumbusha wazazi na walezi kuwa mtoto hajawahi kukua kwa mzazi wake hivyo wasichoke kuwafundisha na kuwakemea pale ambapo wanaenda kinyume na maadili ya nchi yetu.

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Polisi Jamii mkoani humo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Fraterine Tesha amesema kuwa kampeni hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwajengea uelewa watoto pamoja na vijana wa Shule za msingi, Sekondari na vyuo vya kati.

  “Napenda kumshukuru Afande Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuruhusu kampeni hii kutekelezwa nchi mzima ambayo kitaifa ilizinduliwa rasmi Agosti 29, 2024 mkoani Njombe hii itasaidia kuwatayarisha vijana wetu ili kujenga Taifa la kizazi chenye maadili mema” alisema ACP – Tesha.

Naye afisa ustawi wa Jamii Halmashauri ya Kishapu ndugu Paul Palaso amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kampeni hiyo ambayo itaokoa jamii kutokana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto,  “tumewahi kuona madhara mengi sana ya ukatili wa kimwili ambao unapelekea vifo na ulemavu wa kudumu kwa watoto wetu pia ukatili unadumaza Taifa hivyo tutumie vyema kampeni hii kuongea na watoto wetu kuwaelimisha na kuwafuatilia kwa ukaribu mienendo yao ili wasije wakaharibiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GIPHY App Key not set. Please check settings

Mhe. Joseph Mkude Mkuu wa Wilaya ya Kishapu 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GIPHY App Key not set. Please check settings

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Fraterine Tesha Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GIPHY App Key not set. Please check settings

Ndugu Paul Palaso Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Kishapu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GIPHY App Key not set. Please check settings

Cpl Gabriel (Nyumbu mjanja) wa kitengo cha Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GIPHY App Key not set. Please check settings

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GIPHY App Key not set. Please check settings

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GIPHY App Key not set. Please check settings

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GIPHY App Key not set. Please check settings

This post was created with our nice and easy submission form. Create your post!

What do you think?

Written by admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GIPHY App Key not set. Please check settings

WATANZANIA WAHIMIZWA KUENZI TAMADUNI ZAO

12

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OCTOBA 20, 2024