Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Onesmo Lyanga Oktoba 12, 2024 ametembelea na kukagua askari wa Operesheni Kambale inayoendelea katika Wilaya ya Tunduru eneo la Kijiji cha Lukumbule na Makande ambavyo vipo mpakani mwa Nchi ya Tanzania na Msumbiji ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma.
Akiwa katika kambi ya askari hao DCP Lyanga aliwasisitiza kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kufanya kazi kwa nidhamu, haki, weledi na uadilifu wa hali ya juu ili wananchi wa maeneo ya mpaka huo yaendelee kuwa salama.
Pamoja na hilo pia aliweza kutembelea na kukagua kituo cha Polisi Lukumbule ambacho kinajengwa kwa nguvu za wananchi kijijini hapo.
This post was created with our nice and easy submission form. Create your post!
GIPHY App Key not set. Please check settings